HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2022

Waziri Mkuu Majaliwa aitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuzisimamia Asasi za Vyuo Vikuu vya Nje

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika banda la Chuo Cha Ardhi kabla ya kufungua rasmi Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na TCU na kufanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

 

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuendelea kuzisimamia kikamilifu Mawakala wa Vyuo vya Nje ili kuhakikisha vijana wanaopata fursa za masomo katika vyuo hivyo wanapata elimu yenye viwango na ubora inayoendana na ushindani wa soko la ndani na nje la ajira.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na TCU yanyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo.

Amesema kuwa wizara hiyo ina jukumu la kuendelea asasi za vyuo vya nje ili kuhakikisha zinapeleka anafunzi kwenye vyuo vinayotambulika na vyenye viwango vya ubora unaohitajika na unaondeana na soko la ajira.

"Wito kwa wizara kuendelea kusimamia asasi za vyuo vya nje ili vijana wanaoenda kusoma vyuo hivyo wapate elimu bora mhakikishe vina viwango na ubora unaotambulika," amesema Waziri Majaliwa.

Ameikumbusha TCU kuendelea kua karibu na asasi hizo kufuatilia miongozo wanayoitoa kwa vijana  wanaotaka kwenda kusoma vyuo vya nje na kwamba vijana hao wanatakiwa kijiridhisha ubora wa vyuo hivyo kwenye orodha ya vyuo ya tume hiyo.

Amezipongeza taasisi za uwakala wa vyuo vya nje kwa kuendelea kuendelea kuisaidia Serikali katika sekta ya elimu kwa kupeleka wanafunzi nje ikiwemo Kampuni ya Global Link Education.

Ameziomba Taasisi za Elimu ya Juu kuendelea kupitia  mitaala na kuanzisha mipya inayoendana inayoendana na soko la ajira huku akivikumbusha kuongeza ubunifu kwenye mitaala ijibu soko hilo la ndani na nje.

Waziri Majaliwa amewaomba Watanzania kujitokeza kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti mwaka huu kwa kutoa ushirikano kwa makarani watakaofika kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Naibu Katibu wa wizara hiyo Profesa James Mdoe amesema wataendelea kusimamia mitaala inayotolewa na vyuo vya elimu ya juu inaendana na soko la ajira na maendeleo ya viwanda.

Pia, amesisitiza kuwa wizara hiyo kupitia TCU itaendelea kuchukua tahadhari ya Uviko-19 ili kuhakikisha vyuo vinaendelea kutoa elimu.

Naye Mwenyekiti wa TCU, Profesa Penina Mlama amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa vyuo vikuu kujitangaza na wananchi kujionea kozi mbalimbali zinazotolewa na vyuo hivyo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla ameipongeza TCU kwa kutatua changamoto zilizokuwa zikivikabili vyuo vikuu na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za mikopo kusababisha kupunguza migomo ya wanafunzi vyuoni.

Katibu Tawala huyo amempongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kusimamia vyema fedha za mikopo zinazotengwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.


No comments:

Post a Comment

Pages