HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2022

Waziri wa Maji SMZ aitaka ZAWA kutafuta mashine ya kusukuma Maji

 Na Talib Ussi,  Zanzibar

Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaibu Hassan Kaduara ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Maji Zanzibar (ZAWA) kutafuta mashine ya kusukumia maji.


Alisema ni lazima mashine hiyo ipatikane haraka ili wananchi wa Kizimkazi Mkunguni waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.
Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea kianzio cha maji katika kijiji cha kizimkazi kifuatia wananchi wa eneo hilo kukabiliwa na changamoto ya huduma hiyo.


Alifahamisha kwamba  ametoa maelekezo hayo kwa sababu ZAWA inauwezo wa kukunua mashine na wananchi wakapata maji.


 “Kama utakumbuka kesi kama hii iliwahi kutokea Jambiani, ZAWA ni mamlaka ya Serikali wanajua wapi watapata mashine ya maji, na Serikali ya Zanzibar haishindi kuwaletea wananchi huduma ya maji kwasababu ya mashine moja kuharibika"alisema.


 Waziri huyo aliyagiza  ZAWA kununua mashine mbili za maji zenye uwezo wa KW 11 ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kupata maji.


 Aidha alisema   tatizo la maji litamaliza hasa baada ya kumalizika mradi mkubwa wa maji ambao unategemewa kuwa na tangi la lita milioni tano kwa mijibu wa watalaamu.


Alisema mradi huo upo katika hatua ya awali na unadhamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lakini akitokea mfadhili Serikali itampokea lengo kuu ni hufikisha huduma kwa wananchi wote wa Zanzibar waondokane na usumbufu wa kutafuta maji.



Naye Mkurugenzi rasilimali Maji kutoka ZAWA Maulidi Hassan Khamis Alisema shinda hiyo ya ukosefu wa mji imekuja baada ya kuungua mashine moja ya kusukumia maji.


Pia alisema mashine iliyopo uwezo wake ni mdogo KW 9.2 ndio maanza watoa maji kwa mgao ili kuipumzisha isijeikaungua na kupelekea wananchi kukosa kabisa maji.


Kwa Upande wake Farida Mohamed Khamis mkaazi wa kijiji hicho, alisema wanapata maji kwa mgao kila baada ya siku mbili jambo ambalo halikidhi mahitaji kutokana na umuhimu wa huduma hiyo.


No comments:

Post a Comment

Pages