Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Mafunzo ya Vitendo kwa Watendaji watakaosimamia Uendeshaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Amebainisha
kuwa maandalizi ya uendeshaji wa treni hiyo yanaendelea vizuri kwani
miundombinu ya kipande cha kwanza kinachotoka Dar es Salaam hadi
Morogoro kimekamilika kwa zaidi ya asilimia 97 huku kipande cha pili
kutoka Morogoro hadi Makutupora kimeshakamilika zaidi ya asilimia 91.
“Haya ni maandalizi ya uendeshaji wa treni ya kisasa ambayo miundombinu yake kwa kipande cha kwanza cha Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika kwa zaidi ya asilimia 97 na kipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutopora kimekamilika kwa zaidi ya asilima 91” amesema Kadogosa.
Amesisitiza kuwa TRC limeamua kuwatumia wataalamu KORAIL kutoa mafunzo hayo kwa watendaji wa TRC kwasababu uendeshaji wa treni ya kisasa Korea ya Kusini ni salama kwa asilimia 99.9 ambapo inaonesha wana wataalamu waliobobea katika nyanja zote za uendeshaji wa treni ya kisasa.
Amezitaja baadhi ya nyanja ambazo wataalamu wa KORAIL watatoa mafunzo ya nadharia na vitendo ni jinsi ya kupanga treni, uongozaji wa treni, uendeshaji wa treni, biashara ya treni, kutoa utaalamu wa karakana ziweje na usafirishaji katika uendeshaji wa treni, na kwamba yatakuwa ni ya kina na yatatolewa kwa muda wa miaka mitatu.
“Ili kupata elimu nje ya muda wa kazi ni vyema kuwa na uhusiano mzuri na wataalamu hawa kutoka KORAIL kwa sababu watakuwa TRC kwa muda mrefu” amesisitiza Kadogosa.
Amefafanua kuwa uendeshaji wa treni ya kisasa utaanza rasmi mwezi Februari mwakani baada ya taratibu zote za majaribio kufanyika na kukubaliana gharama za usafirishaji na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini( LATRA).
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi kutoka KORAIL, Lee Seung Young ameushukuru Uongozi wa TRC kwa kuwaamini kwa kazi ya utaoaji mafunzo kwa vitendo katika uendeshaji wa treni ya kisasa na kuahidi kutoa mafunzo kwa ufanisi kwasababu wamekuja na wataalamu katika nyanja mbalimbali na wana uzoefu wa kutosha kwenye uendeshaji wa treni ya kisasa.
Mafunzo kwa vitendo kwa uendeshaji wa treni ya kisasa yatashirikisha watendaji vijana zaidi ya 30 kutoka TRC na wataalamu 15 kutoka KORAIL.
No comments:
Post a Comment