HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2022

Wizara ya Fedha na Mipango yatoa ufafanuzi msamaha wa tozo, yasisitiza kuanza kutumika Oktoba Mosi

 

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Wizara ya Fedha na Mipango imetoa ufafanuzi kuhusu Msamaha wa tozo uliosomwa Bungeni Mjini Dodoma Septemba  20 mwaka huu, na Waziri wa wizara hiyo DKt. Mwigulu Nchemba na kusisitiza  kuwa utaanza kutumika Oktoba Mosi, 2022.


Akizungumza na wanahabari jijini humo Kamishna Msaidizi Uchambuzi wa Sera Wizara ya Fedha na Mipango William Mhoja amesema kuwa Serikali imefuta tozo  kuanzia shil 0 hadi sh 30,000 na kwamba itakayozidi kiwango hicho itatozwa makato yaliyozoeleka awali.


Amebanisha kuwa, katika ufutaji wa tozo na utoaji wa msamaha wa tozo hizo umezingatia hatua zote za kuwashirika wadau wakiwemo wamiliki wa mabenki na mitandao ya simu pamoja na kuangalia watumiaji wa kawaida wakiwepo Wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) .


Amesisitiza kuwa Serikali kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu itafuta na kusamehe tozo kuanzia asilimia 10 hadi 50, huku akibainisha kuwa utozaji wa tozo hizo si adhabu bali ni kwa ajili ya kuendesha Serikali.


"Serikali imepunguza wogo wa tozo, kuchochea matumizi ya miamala kwa ajili ya kupunguza fedha taslimu katika kurahisisha utozaji na kuzuia kutoza fedha mara mbili"amesema Mhoja .


Ameongezo kuwa marekebisho yaliyofanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote na kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya Benki, ambapo marekebisho mengine ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki nyingine pande zote .


Pia  amesema Serikali imesamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wa fedha kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi  Sh 30,000, ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu ch Sh 10,000 hadi kiwango cha juu Sh 7,000.


No comments:

Post a Comment

Pages