HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2022

AZAM FC, TP MAZEMBE NGOMA SARE



Na John Marwa


KIKOSI cha Azam FC kimetoshana Nguvu na miamba ya Soka la Afrika Klabu ya TP Mazembe mchezo wa kirafiki uliopigwa Ndola nchini Zambia.


Azam na Mazembe wamehitimisha dakika 90 za mchezo wa kupimana Nguvu kwa sare ya (1-1) mtanange uliokuwa kwa ajili ya kuimarisha vikosi vya Klabu zote mbili kuelekea michezo ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho CAFCC.


Bao la Azam FC limewekwa kambani na Kipre Junior kabla ya Ze Manga Soze kusawazisha kwa upande wa TP Mazembe.


Azam ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo wanajiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC ambapo wao watakutana na Al Akhdar.


Mazembe wao wanajiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa CAFCL dhidi ya Vipers ya Uganda.


Ulikuwa mchezo wenye ushindani kwa pande zote mbili, ulijaa Ufundi mbinu na Ubora wa wachezaji wa vikosi vyote viwili.

No comments:

Post a Comment

Pages