Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, akipata
maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Injinia Cyprian Luhemeja ,
alipotembelea banda la Dawasa wakati wa maonesho ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani.
Na Victor Masangu,Pwani
Mamlaka
ya maji Safi na usafi wa mazingira (DAWASA) imeahidi kuendelea
kuboresha na kufikisha huduma ya maji kwa wawekezaji mbali mbali wa
viwanda vidogo na vikubwa lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali
katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.
Hayo
yamebainishwa leo na mtendaji mkuu wa Dawasa Injinia Cyprian Luhemeja
wakati akitoa taarifa kwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Dawasa wakati wa ufunguzi rasmi wa
maonesho ya tatu ya uwekezaji na biashara Mkoa wa Pwani.
Alisema
kwamba lengo lao kubwa ni kuweza kuboresha zaidi huduma ya maji kwa
wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani ikiwemo
wawekezaji wa viwanda vyote kuwapatia huduma ya maji.
"Tumeshiriki
katika maonesho haya kwa lengo la wananchi waweze kufahamu utekelezaji
wa majukumu yetu mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyafanya katika mikoa
ya yetu ya Dar es Salaam pamoja na Pwani na tunawahidi kuwaboreshea
huhuma ya maji kuanzia ngazi za vitongoji,"alisema Luhemeja.
Aidha
Luhemeja amesema kuwa hakuna tatizo la maji kutokana na mitambo yote ya
ruvu chini pamoja na ule wa ruvu juu yote inafanya kazi vizuri na
kwamba wameshakukua tahadhari endapo kama kukitokea na ukame.
Kadhalika
alisema miradi mbali mbali kwa ajili ya usambazaji wa maeneo tofauti
bado kazi inaendelea ikiwemo Sambamba na kuchimba mabwawa ambayo
yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha ukame wa mvua.
Kwa
upande wake Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete aliupongeza
Mkoa wa Pwani kwa kuandaa maonesho hayo ambayo yataweza kutoa fursa ya
wafanyabiashara kuonesha bidhaa wanazozizalisha.
Kadhali
alimpongeza mtendaji mkuu wa Dawasa kwa kuweza kuendelea kuwahudumia
wananchi katika kuwasambazia maji safi na salama ili wananchi waweze
kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.
No comments:
Post a Comment