HABARI MSETO (HEADER)


October 29, 2022

YANGA SC BADO SANA KUPOTEZA MCHEZO


Na Mwandishi Wetu

Mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga SC wameendeleza wimbi la kutopoteza mchezo ikiwa ni mchezo wa 45 sasa.

Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao (0-1) mbele ya Geita Gold FC mchezo uliolondima jioni ya leo katika dimba la Kirumba jijini Mwanza.

Geita Gold waliwapa mechi nzuri sana Yanga, Fred Minziro alikuwa na mpango sahihii ila kuna nyakati aliangushwa na ubora wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa vijana wake.

Geita bila mpira walikuwa na umbo la 4-4-2, Saido na Lyanga mbele ya Job na Bacca na nyuma ya Mauya na Feisal, lengo, kuinyima Yanga utulivu wakati wa kujenga mashambulizi.

Wakati ambao Bacca na Job wanaanzisha mashambulizi walikosa machaguo sahihi ya pasi kwenda kwenye eneo la kiungo, Saido na Lyanga wanatanuka ili kuziba njia za mipira kutoka chini kwenda mbele.

Hii ilipelekea Mauya kushuka chini na kusababisha timu ifanye ianzishe mashambulizi  na wachezaji watatu ( Job, Bacca na Mauya ) kitu ambacho kiliwafanya Yanga kupunguza mchezaji mmoja kwenye eneo la kiungo baada ya Mauya kushuka chini.

Dakika ya 44 Mwamuzi Florentina Zabron aliwazawadia Yanga mkwaju wa penati kwa kuamua kuwa mlinzi wa Geita aliunawa mpira ikiwa tukio hilo limefanyik nje ya boksi la  18.

Hadi mwisho Yanga wanafanikiwa kuibuka na point tatu kwa bao moja kwa bila.

Yanga wanafikisha point 20 mara baada ya kushuka Dimbani mara nane mpaka sasa na kukaa kileleni huku wakifikisha michezo 45 bila kupoteza katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

Pages