HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 14, 2022

YANGA SC: TUNAOMBA RADHI

 


Mfungajai wa bao la Yanga, Clement Mzize.

 

 Na Mwandishi Wetu


Licha ya kuibuka na pointi tatu muhimu Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Nasriddine Nabi amewaomba mashabiki wa Yanga msahama kwa kikosi chao kushindwa kuonyesha kabumbu safi.


Yanga wameshuka Dimbani dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushidi wa bao moja kwa bila.


Nabi amesema ulikuwa mchezo mgumu sana kwao na kikubwa kilchokuwa kinahitajika ni pointi tatu kisha mengine yatafuata.


"Kwanza tunaomba radhi kwa mashabiki wetu kwa mchezo mbaya tuliouonyeaha leo, ratiba imekuwa ngumu sana kwetu hivyo kikubwa tumepata pointi tatu mengine tutaenda kuyatazana kwenye Uwanja wa mazoezi.


"Niwapongeze Kagera wamecheza vizuri sana na kutuuliza maswali magumu lakini bahati imekuwa kwetu jioni ya leo" amesema Nabi.


Ni pointi tatu ngumu kwa Wananchi, kitu kilihotegemewa na wengi hata  ingekuwa ni kuchagua moja wapo kati ya kiwango kizuri na matokeo hakika Mwanayanga yeyote angechagua matokeo mazuri na ndicho walichokipata Yanga katika mchezo wa leo.


Kiufundi kocha Nabi aliingia kwa lengo la kutegemea zaidi kushambulia kwa mipira ya krosi, mazingira ya uwanja  yakamlazimisha kuingia na mfumo wa 3-5-2 lengo ni kuwa na washambuliaji wawili mbele ambao wataishinda mipira ya juu inayotoka kwenye mapana ya uwanja.


Yanga ilikosa ufanisi kutokana na mpango wa Kagera Sugar kuwa bora katika kuutawala mchezo katika maeneo yote ya Uwanja, Licha ya  wachezaji wengi wa Yanga kukosa makali yao.


Ubora wa Kagera Sugar ulianza kwenye mfumo wao wa  4-3-3,  wanapokuwa na mpira, Anuar, Mbaraka na Mwijage katika mstari wa kushambulia huku wakifanya matendo mengi sahihi kabla ya mipira kuwafikia washambuliaji.


Kagera hawakutaka kushindana na Yanga katika eneo la kati, walisafilisha mipira kona nyingi katika mapana ya kushambulia.


Yanga wameshinda mechi ngumu, Kagera Sugar walikosa umakini katika kumalizia nafasi nyingi walizozitengeneza. Clement Mzize na ufunguo wa bahati katika kufuli gumu la pale Kirumba anaweka bao kali sana na kuihakikishia usalama wa pointi tatu Yanga SC.

No comments:

Post a Comment

Pages