Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji NICOL, Dkt. Gideon Kaunda akizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa Nane uliofanyika katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere.
Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji NICOL wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye Mkutano Mkuu wa Nane wa kampuni hiyo uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salam.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Gawio hilo lilipitishwa siku ya Jumamosi katika maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa mwaka wa wanahisa uliofanyika kwa njia ya video kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Hayo yamesemwa jijini humo baada ya mkutano huo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa NICOL, CPA Erasto Ngamilaga na kwamba mkutano mkuu ambao umefanyika ni takwa la kisheria kwa makampuni kama hayo kufanya na wanahisa wake wote.
Amesema kuwa kwenye mkutano huo wamehudhuria wanahisa wa mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam ambapo wale wa mikoani walifuatilia mkutano huo kwa njia ya mtandao.
Amesisitiza kuwa kwenye mkutano huo wamepata fursa ya kuwaeleza wanahisa namna kampuni ilivyopata faida ya Sh bilioni nne kabla ya kodi na Sh bilioni 3.8 baada ya kodi.
Ameongeza kuwa wanahisa wamepitisha gawio la Sh 20 kwa kila hisa ambayo itaanza kulipwa Disemba 15 kwaka huu na kwamba ni ongezeko la gawio la Sh 17 ambalo lilishalipwa kwenye mahesabu ya mwaka 2021.
“Wanahisa wamefurahi sana kuona kampuni inafanya vizuri na sisi viongozi tumewaaahidi kuweka mikakati mizuri zaidi kuhakikisha kampuni inazidi kusonga mbele na kupata faida kubwa zaidi siku za usoni,” amesema Ngamilaga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NICOL, Dkt. Gideon Kaunda, amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa gawio kila mwaka na ameishukuru bodi mpya kwa kuwekeza sehemu mbalimbali hasa kwenye hati fungani za serikali.
Amefafanua kuwa kampuni hiyo imewekeza asilimia 30 ya uwekezaji wake kwenye hati fungani na ndiyo sababu kampuni hiyo imeendelea kupata faida mwaka hadi mwaka na kuwapa gawio zuri wanahisa wake.
Ameongeza kuwa wanahisa wa NICOL nchi nzima wanafikia 30,000 na wamesambaza sehemu za mikutano ili kuwafikia wanachama wengi badala ya kulazimika kuja Dar es Salaam kwenye mKutano Mkuu wa mwaka.
“NICOL inapenda kuona wanahisa wake wanapata gawio kila mwaka na kweli kampuni imefanya vizuri na gawio limeongezeka kutoka Sh 17 na sasa tutalipa sh 20 kiwango ambacho kampuni zingine zimeshindwa kufikia na tunadhani mwakani tutazidi kuongez gawio kubwa zaidi kwa wanahisa wetu,” alisema.
Nae, Mwanahisa Mutamwega Mugaywa, amesema anashukuru kuona kampuni ya NICOL imesimama na kuonyesha matumaini makubwa kwa wanahisa wake.
“Nifuraha kubwa kuona NICOL inabeba uchumi na nawashauri watu wengine waje wanunue hisa zao mapema NICOL kwasababu kuna faida nyingi kuwa mwanahisa wakampuni ya wazalendo,”
“Nawapongeza viongozi kwa kusimamia vizuri Kampuni na sasa tunapata gawio zuri nawashauri wengine nao wachangamkie hisa za kampuni yetu,” amesema.
Mwanahisa mwingine, Suzana Masele amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Dk. Kaunda kutokana na anavoisimamia kampuni hiyo na menejimenti nzima.
“Nampongeza kwani anavyoisimamia vizuri kamouni utadhani ni kampuni yake binafsi ukiangalia ilipokuwa huko nyuma ilikuwa kama imekufa lakini mwenyekiti wa sasa anajua anachofanya na tunaelekea pazuri zaidi,” amesema
No comments:
Post a Comment