Na John Richard Marwa
Wakati leo wakitarajiwa kushuka dimbani Mabingwa watetezi wa Ligi Soka Tanzania Bara Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Kocha Mkuu Nasriddine Nabi amelia na ugumu wa ratiba inayowakabili.
Yanga walitua juzi kutoka Tunisia ambako walikuwa kwenye uwakililishi wa nchi katika mchezo wa pili kuwania kufuzu Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC dhidi ya Club Africain
Katika mchezo huo Yanga walifanikia kuibuka na ushidi wa bao moja kwa bila nabkufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya CAF CC.
Baada ya kutua jijini Mwanza Kocha Nabi amesema ratiba yao ni ngumu sana.
“Ratiba yetu ni ngumu sana. Tumemaliza muda mwingi kwenye ndege kuliko uwanja wa mazoezi. Tangu jumatano hatujafanya mazoezi kujiandaa na mchezo huu.
“Tumefika Mwanza jana 7 usiku na tuna siku moja tu ya mazoezi. Hii sio rafiki kwa afya ya mwili wa wachezaji." amesema na kuongeza kuwa.
"Hatuko hapa kulalamika lakini tunaamini viongozi wa mpira wetu jambo hili kwa wakati mwingine wanatakiwa kulitazama kwa jicho tofauti. Tulikwenda Tunisia kuiwakilisha Tanzania.”
Ikumbukwe kuwa Yanga wanashuka kwenye mchezo wa leo wakiwa wamecheza michezo 45 ya Ligi bila kupoteza na kama leo watashinda basi wataendeleza wimbi la ushidi wa 46.
Na kama watapoteza basi wtakuwa wanaandik a rekodi mpya baà da ya dakika 4050 bila kupoteza mchezo.
No comments:
Post a Comment