HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2022

SIMBA SC TATU KAPUNI

Pape Sakho akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara dhidi ya Ihefu FC.


Na Mwandishi Wetu

Wekundu wa Msimbazi Simba wameondoka na pointi tatu muhimu dhidi ya Ihefu FC kwenye Dimba la Benjamin Mkapa mchezo wa Ligi  Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL).

Mechi ngumu kwa Simba licha ya umiliki mkubwa wa mpira, ni kama vile Simba bila Chama hakuna hatari walyonayo kivipi?

Ukitazama dakika 45 za kwanza Simba wanachukua mchezo kwa asilimia 78 kwa 22 za Ihefu lakini hakuna hata mashuti matatu yaliyolenga lango ni hatari isiyo na madhara.

Kukosekana kwa Chama Simba imepoteza sura halisi yà kushambulia kwa mipango. Agustin Okrah, Pape Sakho wanaikosa pasi ya mwisho ya hatari kwenda kwa Moses Phiri na Habibu Kyombo.

Hata pale timu inapotengeneza nafasi bado utulivu unakosekana kwa washambuliaji kwa kukosa ufanisi wa kuzitumia hizo nafasi.

Licha ya kuwa Ihefu walikuwa na mpango kazi mzuri wa kuzuia kwa kucheza na idadi kubwa ya wachezaji nyuma ya mpira kwenye mistari miwili ya kiulinzi wanne kwa watano bado kuna nyakati walitoa mianya kwa mlinda mlango wao kufikiwa.

Pape Sakho nakubali kunyanyua kidole chake na kuhesabiwa kwa kutandika shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Phiri dakika ya 63.

Hadi dakika 90 za mchezo zinatamatika Simba SC (1-0) Ihefu. Kwa matokeo hayo Simba inafikisha pointi 21 michezo 10 nafasi ya pili nyuma ya vinara Azam FC wenye pointi 23 michezo 11.

Ihefu FC wanaendelea kusalia mkiano mwa msimamo wa NBC PL Ika hawajafikisha hata pointi 10 katika mchezo 10 .

No comments:

Post a Comment

Pages