HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 24, 2022

 Rais Samia amwaga mabilioni kwa wasanii

Na John Mapepele


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa hundi za mamilioni ya fedha kwa wadau waliokidhi kukopa kwenye mfuko wa Utamaduni na Sanaa na amewataka wasanii na wadau wa kazi za sanaa kujitokeza kwa wingi kuomba  kukopeshwa  fedha  kutoka kwenye  mfuko huo alioufufua Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.



Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Disemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam  akiwa na Katibu Mkuuwa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kwenye uzinduzi rasmi wa utoaji mikopo kutoka kwenye mfuko huo ambapo uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na  viongozi na wadau mbalimbali wa Sanaa  na Utamaduni.

Aidha, wakati wa uzinduzi huo wadau wa tano kati ya  kumi na tisa waliowasilisha maombi yao walipatiwa fedha  za mfuko huo.Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samiaa ni kuona kuwa kila Mwananchi (msanii au mdau wa sanaa) mwenye sifa ya kukopa kwenye mfuko aweze  kupata fedha  ya kuboresha kazi zake.

“Naomba  nieleweke  vizuri fedha hizi ni za  kila  mtanzania, kila mwana sanaa, kila Kijiji, kila kata, kila wilaya, kila mkoa, yule ambaye anaamini ana kazi yake ameitengeneza, yule ambaye anaamini ameandaa muswada  wake vizuri, awe Tanga awe Dodoma  awe songea, awe Mtwara atazipata ikiwa  tu ana sifa” amefafanua  Waziri Mchengerwa.

Amelielekeza Baraza la Sanaa nchini kuandaa  utaratibu wa kutengeneza mfumo ya kimtandao ambao utawafanya waombaji  kutoka sehemu mbalimbali nchini kuweza kuomba  wakiwa  huko huko na kupatiwa  huduma  badala ya kusumbuka kuja Dar es Salaam.

Awali amewataka watendaji  kujiongeza kwa kushirikiana na wadau ili kupata fedha zaidi za kuwasaidia wasanii ili waweze kuwakopesha  viwango  vikubwa ambavyo vitakidhi  matakwa  ya waombaji  hao.Katika  uzinduzi  huo Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan  Abbasi alimtambulisha Mtendaji  Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni Sanaa, Bi.Nyakaho Mturi Mahemba

No comments:

Post a Comment

Pages