Na Mwandishi Wetu
BARAZA
la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)
limefungua dirisha la udahili wa mkupuo wa mwezi Machi kwa mwaka wa
masomo wa 2023/24 kuanzia Januari 16 mwaka huu.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo imesema kwamba
vyuo vyote vinaruhusiwa kudahili wanafunzi katika mkupuo huu, isipokuwa
vyuo vinavyotoa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa Tanzania
Bara.
Taarifa
hiyo imesema vyuo vya Afya na Sayansi shirikishi vilivyopo Tanzania
Visiwani vyenye uwezo wa kudahili katika mkupuo huo vinaruhusiwa ikiwa
vitakidhi vigezo.
Katika
taarifa yake hiyo, NACTVET limevielekeza vyuo vinavyohitaji kudahili
wanafunzi kwa mkupuo huu kutuma maombi yao kabla ya Januari 27, 2023 kwa
kujaza fomu inayoonesha uwezo wa chuo kuendesha mafunzo na kuiwasilisha
katika ofisi za Kanda za Baraza ambapo chuo husika kipo.
“Uwezo
huo ni pamoja na kuwa na miundombinu na walimu wa kutosha kutoa mafunzo
katika mikupuo miwili kwa mwaka (Machi na Septemba)” imesema sehemu ya
taarifa hiyo.
Baraza hilo limesema kwamba fomu ya maombi inapatikana katika tovuti ya Baraza hilo www.nacte.go.tz kwa kubofya fomu ya maombi ya udahili March Intake 2023/24.
No comments:
Post a Comment