HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2023

  JATU PLC yatangaza Mabadiliko Makubwa ya Kiutendaji


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kampuni ya JATU PLC  imetangaza kuwa imerejesha shughuli za  Makao yake Makuu Jijini Dar es Salaam kutoka Wilayani  Sumbawanga,Mkoani Rukwa zilikoahamishiwa mnamo mwaka jana. 
 
 
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Simbano alipokuwa Akizungumza na wanahabari jijini humo juu ya ujio wa Mtaalamu wa Masuala ya Fedha, Miradi na Biashara kutoka Nchini Uholanzi ambaye atakuwepo nchini kwa majuma mawili kusaidia kampuni hiyo kutengeneza  mpango kazi mpya wa biashara itakayoendana na dira na maono ya kuanzishwa kwa JATU PLC.

Amesema kuwa tangu kampuni hiyo ilipofanya mabadiliko ya uongozi mwezi Agosti mwaka jana wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kuirejesha kampuni hiyo ambayo ilipitia changamoto mbalimbali na tayari wamesharudisha baadhi ya huduma za uzalishaji wa unga wa Dona na Sembe katika ofisi zao ndogo zilizopo Kinyerezi Jijini hapa.

"Ndugu wanahabari kwasasa tumewekeza nguvu kubwa zaidi shambani  mwaka huu wa 2023 ili kuongeza mapato zaidi na spidi ya kupunguza madeni pia tumerudisha ofisi zetu za makao makuu hapa jengo la PSSSF HOUSE" amesema Simbano. 

Akizungumzia Kuhusu ujio wa mtaalamu huyo wa masuala ya fedha miradi na baishara kutoka nchini Uholanzi, Simbano amesema kuwa mgeni huyo aliyeingia nchini January 2 mwaka huu kwa ushirikiano wa taasisi ya PUM Netherlands Senior Experts ataungana na wataalamu wa masuala ya fedha na mitaji ambao ni Luzane Financing na Kampuni ya Ushauri wa Kibiashara ya InterCapital kwa kushirikiana na SSS Capital zote kutoka Tanzania na watafanya kazi ya kuandalia kampuni ya JATU PLC mpango kazi mpya wa biashara, kushauri juu ya mabadiliko yanayoendelea.

Kazi nyingine zitakazofanywa kwa ushirikiano wa makampuni hayo ni pamoja na kushauri juu ya kukuza mtaji na kulipa madeni yote kwa kuketi chini na wadai wote kuona namna ya kuendesha miradi iliyokuwepo kuisimamia kwa weledi na ujuzi ili kuleta tija na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zilizojitokeza.

Amebainisha kuwa  kampuni hiyo itashirikisha wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ambao ni wanahisa, wakulima, washauri, taasisi za kiserikali na wahisani ili kuweza kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya uongozi wa JATU PLC.

Kwa upande wake,mtaalamu huyo, amepongeza mfumo wa uendeshaji wa biashara wa Kampuni ya JATU PLC na kuongeza kuwa mfumo huo utakuwa madhubuti zaidi endapo utasimamiwa vizuri.

Ameongeza kuwa katika siku 14 atakazokuwa hapa nchini kama sehemu ya jopo la washauri atahakikisha kampuni hiyo inafikia malengo ya uanzishwaji wake Kwa kufikia hatua nzuri itakayotatua changamoto zote kibiashara kwa kuboresha uwekezaji wake.

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya JATU PLC, Mhandisi  Dkt. Zaipuna Yonah  amewaondoa hofu Watanzania juu ya kampuni hiyo na kusema kuwa mabadiliko makubwa ya uongozi yaliyofanywa mwezi Agosti mwaka 2022 yatahakikisha maono ya kampuni hiyo yanafanyiwa kazi kwa weledi mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages