HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2023

MAPINDUZI NA MLANDEGE CHITAKI

Na John Richard Marwa


Ukisikia Zanzibar imesema 'CHITAKI' kusikia kombe linavuka maji ndio hii. Klabu ya Mlandege imetwazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi makala ya 17 baada ya kuwachapa Singida Big Stars mabao (2-1).


Imekuwa Fainali bora na nzuri ya kutazama kwa namna timu zote mbili zilicheza kuusaka ubingwa mbele ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hussein Ally Mwnyi.


Mlandege waalianza kwa kasi kulishambulia lango la Singida Big Stars na kufanikiwa kujipatia mabao mawili ndani ya dakika 20 za mwanzo kabla ya Singida Big kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Fancy Kazadi kipindi cha pili.


Singida Big Stars licha ya kufanya mabadiliko kadhaa lakini walishindwa kufua dafu mbele ya vijana wa Mlandege.


Hakika Mlandege wanakuwa timu pili kutoka Zanzibar kutwaa taji hilo tangu kuanzishwa kwake miaka 17 iliyopita.


Mlandege wamesema hatutaki kuwa wateja, hatutaki  kuwa wasindikizaji wa mchuano hii ambayo tunaiandaa wenyewe. Naaam CHITAKI imekubali mbele ya Rais wa Zanzibar na wazanzibari wamefurahi.

No comments:

Post a Comment

Pages