HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2023

SIMBA SC YAPOTEZA KWA AL DHAFRA ABU DHABI


Na Mwandishi Wetu


Klabu ya Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya wenyeji wao Al Dhafra ya Falme za Kiarabu Dubai uliofanyika jioni ya leo mjini Abu Dhabi.



Huu ni mchezo wa kwanza wa Simba ndani ya Falme za Kiarabu ambako wameweka kambi ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL na mashindano mengine yakiwema ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL chini ya Kocha Mkuu Robertinho Oliveira.


Hadi dakika 45 za kwanza zitamatika mchezo huo ulikuwa suluhu huku Kipindi cha pili makosa ya safu ya ulinzi yakiwapatia Al Dhafra bao la kuongoza na la ushindi.


Simba watashuka dimbani tena Januari 15 kuwakabili Mabingwa wa zamani wa Ulaya klabu ya CSKA Moscow ya Urusi, mchezo ambao pia utafanyika katika mji wa Abu Dhabi.

No comments:

Post a Comment

Pages