Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa
Mkoa huo Peter Serukamba alipokutana na Maafisa elimu na wakuu wa Wilaya ili
kujadili hali ya usaili wa wanafunzi
mashuleni.
Amesema idadi ya wanafunzi wa Sekondari walioripoti mashuleni ni ndogo
ikilinganishwa na uwingi wa madarasa yalijengwa na Serikali hivi karibuni hivyo
ni jukumu la Maafisa elimu hao kuhakisha wanasakwa popote walipo na wapelekwe
shuleni.
RC Serukamba ameendelea kueleza kwamba ifikapo Siku ya jumatatu tarehe 23
January 2023 anataka taarifa ya kutoka kila kata kuhusu wanafunzi wangapi wamesajiliwa na
wangapi bado na Sababu za kutosajiliwa.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi Mkoani Singida kuhakikisha hakuna
Mtoto aliyechaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza atakayebaki nyumbani.
"Nimejiridhisha kwamba hali ya usaiili wa wanafunzi wa kidato Cha
kwanza inasuasua Sana, Serikali imejenga madarasa ya kutosha,imefuta Ada
mashuleni lakini bado wapo wazazi hawawapeleki watoto wao shuleni hili
halitakubalika" Serukamba.
Kwa upande wake DC wa Iramba Suleimani Mwenda amesema bado Katika Wilaya
yake bado hali ya kujiunga na kidato Cha kwanza unaenda kwa kusuansua Jambo
ambalo waliamua kuchukua hatua kwa kuwaita wazazi na wanafunzi ofsini kwake ili
kuwasikiliza.
DC Mwenda anasema amebaini kwamba wapo wazazi wanaozuia watoto kwenda shule
ili waweze kujiunga na Shughuli za kiuchumi za kulima kuchunga mifugo na bà adhi
Kutafuta ajira binafsi.
Mwenda amesema wanapenda kutumia mbinu zote zikiwemo kuwashawishi kutumia
Dola kuwapeleka shule na kuwachukulia hatua wazazi Watakao bainika kuwazuia
watoto kwenda shule.
No comments:
Post a Comment