HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2023

 YAMETIMIA MSIMBAZI, MBRAZIL ATUA NA SAMBA

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Simba rasmi imemtambulisha kocha raia wa Brazil, Robertinho Oliveira kuwa Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi ikiwa ni sehemu ya kuboresha benchi la Ufundi.

 

Zoezi hilo limefayika mchana huu jijini Dar es Salaam ambapo Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi kuwa kuongezeka kwa Kocha huyo ni kuboresha benchi la Ufundi na kuongeza nguvu ya kiufundi kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL hatua ya makundi.

Kocha Oliveira amejiunga na Simba ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu aachane na waajiri wake wa zamani klabu ya Vipers ya Uganda.

Taarifa za kujiunga na Simba zilivuma takribani majuma mawili sasa na hatimaaye yametimia kwa Kocha huyo kuwa ndani ya mitaa ya Msimbazi kwa kandarasi ya miaka miwili.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amebainisha kuwa Kocha Oliveira amekuja kuongeza nguvu kwenye benchi lao akisaidiana na Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake waliopo sasa.

Ikumbukwe kuwa Simba wanafanikiwa kumpata Kocha kutoka kwa wapinzani wao Vipers ambao wako kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL ambapo michezo ya hatua hiyo itaanza kulindima mwezi ujao.

Kocha Oliveira ataungana na timu visiwani Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi msimu huu wa 2023, huku Simba wakiwa Mabingwa watetezi wa kombe hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages