Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Benki ya Mwanga Hakika, Projest Massawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wateja wa kati na wadogo Benki ya Mwanga Hakika, Joseph Samson (katika) akizungumza na waandishi wa habari.
Na Janeth Jovin
WAFANYABIASHARA na wajasiriamali mbalimbali nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kuweka akiba katika benki ya Mwanga Hakika ili waweze kupata asilimia 12 ya faida kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa katika benki hiyo ya Mwanga Hakika, Projest Massawe wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya benki hiyo iitwayo 'Jipange sasa Maisha ni Mseleleko'.
Massawe amesema ili kuhakikisha wanawafikia wateja wengi zaidi beki imeamua kima cha chini cha uwekezaji ni kuanzia Sh. 500,000 na kuendelea na kwamba kila kiwango atakachoweka mteja kitampati fursa ya kupata faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
"Mteja atakayeweka amana katika benki yetu kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 atapata faida mpaka asilimia 12 kwa mwaka, tumekuja na kampeni hii ya Mseleleko Akaunti ambayo itakuwa ya miezi mitatu tunategemea tutawagusa watanzania wengi kwenye hii fursa ya kuweka akiba katika benki yetu na kupata gawio au faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha mwaka mmoja," amesema
Amesema benki hiyo ambayo kwa sasa ina matawi saba nchi nzima, itaweza kuwahudumia watanzania wote hata wale ambao bado matawi hayajafika kwa kutumia mtandao na simu banki.
"Mkakati wetu ni kuwekeza kwa wafanyabiashara na ndio maana tupo hapa kulihamasisha kundi hilo kuja na kupata faida ikiwemo ya kupata mkopo hadi asilimia 80 ya fedha ambayo amewekeza hapa kwetu," amesema Massawe
Aidha amesema anaishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi za kifedha ikiwemo benki yao kuweza kuwahudumia wateja mbalimbali na kuwasaidia kuweza kukuza uchumi wao kupitia uwekezaji.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara Wateja wa kati na wadogo katika benki hiyo, Joseph Samson amesema kwa mfanyabiashara au mjasiriamali atakayeweka akiba katika benki yao, moja ya kigezo anachotakiwa kuwa nacho ni awesome mtu anayefanya shughuli inayokubalika na serikali.
"Pia atatakiwa kuweka kiasi hicho cha Sh. 500,000, fedha zake ziwekwe kwa muda usiopungua miezi sita pamoja na awe amefungua akaunti hii ya Mseleleko, anayehitaji huduma hii tutamfua hata nyumbani kwake kumuhudumia,".
No comments:
Post a Comment