HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 19, 2023

NMB yang'ara tuzo za Umahiri za PRST

 

Kaimu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika (kushoto), akipokea tuzo ya  Afisa Uhusiano Bora 2022 kutoka kwa mmoja wa majaji wa tuzo hizo, Daniel Mshana, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri zilizotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu). 

Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Grace Ngailo akimkabidhi tuzo Kaimu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika (kulia), wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri zilizotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika (kushoto), akipokea tuzo ya taasisi bora katika Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Sarah Kibonde, wakati wa hafla ya
utoaji tuzo za Umahiri zilizotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) 2022 jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kundo Andrew Matthew (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Umahiri za PRST.

No comments:

Post a Comment

Pages