Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE wameweza. Ndivyo unaweza kuelezea mara baada ya Mabingwa wa Kihistoria Yanga SC kuvunja mwiko mbele ya miamba ya Afrika TP Mazembe mchezo wa pili wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC kwa kuibuka na ushindi wa mabao (3-1).
Yanga wameshuka dimbani jioni ya leo kumenyana na Kunguru hao wa Lubumbashi na kufanikiwa kuwadhibiti vile walivyopenda Wananchi.
Mchezo huo ulikuwa mkali na mzuri kwa timu zote mbili kuonyeshana umahili wa kusakata gozi la Ng'ombe na yanga kuibuka miamba jioni ya leo.
Yanga walianza mchezo huo kwa kasi ya kulisakama lango la TP Mazembe katika dakika 15 za kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Kennedy Msonda na Mudathir Yahya.
Kipindi cha pili Mazembe walikuja juu kutaka kuzlsawazisha hadi dakika ya 77 kupata bao kwa mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari.
Wakati Mazembe wakiamini wanaweza kupata alama ndani ya Benjamin Mkapa Yanga walifanya shambulizi la kujibu na kujiandikia bao la tatu kupitia kwa Tuisila Kisinda.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kukusanya point tatu muhimu wakishika nafasi ya tatu mara baada ya US Monastiry kutoka sare dhidi ya Real Bamako ya Mali.
No comments:
Post a Comment