HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2023

Kukamilika kwa Barabara ya Lusahunga-Rusumo kutakuza uchumi wa wananchi

 Na Alodia Babara, Ngara


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Logatus Mativila amesema kwa kipindi cha miaka mitatu Barabara ya Lusahunga hadi Rusumo mkoani Kagera yenye urefu wa KM 92 imekarabatiwa kwa shilingi bilioni 33.



Mtendaji huyo wa Tanroads Mativila ameyasema hayo  Februari 18, 2023 katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya rami yenye urefu wa KM 92 kutoka Lusahunga hadi Rusumo itakayogharimu sh 153.5 billion hafla iliyofanyika kijiji cha Benako wilaya ya Ngara mkoani Kagera.


"Barabara hii ilikuwa na hali mbaya kiasi cha kupitika kwa taabu sana, kukwamisha magari na kusababisha ajali mara kwa mara, ukarabati ndani ya miaka mitatu umegharimu Sh. 33 .67 billion" Amesema Mativila


Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa mpya za kibiashara na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na hivyo kukuza uchumi kwa wananchi wa maeneo hayo na Tanzania kwa ujumla na itachochea shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara, mazao ya misitu, uvuvi na katika shughuli za utalii katika mbuga za Taifa za Burigi na Rubondo mikoa ya Kagera na Geita, muda wa utekelezaji wake ni miezi 24.


Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuanzia Desemba mwaka jana hadi Januari, 2023  miradi ya barabara yenye thamani ya sh 405 billion imesainiwa mikataba hapa nchini.


Prof. Mbarawa amewataka wakandarasi watakaosimamia mradi wa Lusahunga hadi Rusumo kusimamia kwa uadilifu ili fedha ya serikali itumike bila ubadhirifu.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka wakazi wa mkoa huo kujiuliza maswali barabara hiyo watanufaika nayo vipi katika kuongeza uchumi wao na hivyo akawataka kutumia akili kuzalisha mazao mbalimbali ambayo watayasafirisha kuyauza nchi jirani za Rwanda, Burundi na DRC Congo na kuongeza uchumi wao.


Justina Ndailagije mkazi wa kijiji cha Benako  amesema ujenzi wa barabara hiyo utamsaidia kuongeza kipato chake katika biashara ya mama ntilie anayofanyia kituo cha magari makubwa ya mizigo kwani madreva wa magari hayo yatakuwa yanasafirisha mizigo kwa wingi.

No comments:

Post a Comment

Pages