Na Irene Mark
MKIOA 15 Tanzania inatarajiwa kupata mvua kubwa kuanzia leo Machi14 na kesho Machi 15,2023.
Mikoa hiyo ni Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma, Ruvuma Mara, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.
Taarifa ya angalizo la mvua hiyo imetolewa leo Machi 13,2023 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuonesha kwamba mvua hiyo itanyesha kwa siku mbili mfululizo.
“Mvua hizo pia zinatarajiwa kunyesha Machi 15,2023 kwenye baadhi maeneo ya mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.
“Zipo athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi hicho hivyo ni vema wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari mapema,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo TMA inawashauri wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa za kila siku ili kujua nini kitatokea wapi na lini.
March 14, 2023
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment