HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 18, 2023

NABI: WANANCHI NJOONI MUONE

Na John Richard Marwa


Wakati Wananchi wa klabu ya Yanga wakisubiri kuino timu yao inatinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC Kocha Mkuu wa klabu hiyo Nassridine Nabi amewaita mashabiki na wapenzi wa Soka nchini kwenda kutinga Robo Fainali.



Yanga watashuka dimbani kesho katika Dimba la Benjamin Mkapa kumenyana na US Monastiry ya Tunisia ambapo kama Yanga watapata matokeo watafuzu moja kwa moja Robo Fainali ya michuano hiyo msimu huu kutoka kundi D.


Nabi amesema amekiandaa kikosi chake vizuri na wachezaji wako tayari kwa ajili ya mapambano ya kuifikisha timu katika hatua inayofuata.


"Mechi yetu ya kesho ni muhimu sana kwa upande wa Young Africans kwa sababu tukipata matokeo tunafuzu Moja kwa moja Robo Fainali, lakini ni mechi ngumu kwa sababu Monastiry hawajaja hapa kutalii.


"Wanakuja kutafuta matokeo Ili waongoze kundi, kwa sababu wakipata matokeo mazuri na bado wana mechi nyingine nyumbani ambayo wakifanya vizuri wataongoza kundi." amesema Nabi na kuongeza kuwa.


"Wachezaji wako tayari tumejiandaa vizuri, morali iko juu sana kwa vijana wangu hivyo tunaamini tutakuwa na mchezo mzuri hapo kesho.


"Ujumbe wangu kwa mashabiki wa Yanga na mashabiki wa mpira, njooni tuujaze Uwanja wa Mkapa kwa sababu nyinyi ni wachezaji wa 12 Uwanjani." Nabi ameendelea kuwa sihi mashabiki kuwa.


"Njooni na mshangilie muda wote wa mchezo hata pale tutakapo kuwa katika wakati mgumu mchezoni basi kelele zenu zitusaidie kuwa hai mchezoni maana kushangilia kwenu huongeza morali.


"Nawapongeza Monastiry ambapo jana wametimiza miaka 100 karne moja tangu kuanziswa kwake, najua watataka kuendeleza sherehe zao kwa kupata matokeo." amesema Nabi


Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa nafasi ya pili kwenye kundi D nyuma ya wageni wao Monastiry ambao ni vinara wa kundi D hilo wakiwa na pointi 10 huku TP Mazembe wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao nne huku Real Bamako wakishika mkia na pointi zao mbili.


No comments:

Post a Comment

Pages