HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2023

Wanaotakiwa kuhama kupisha Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi Waahidiwa kulipwa Fidia

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Wakazi wanaotakiwa kuhama katika Bonde la Mto Msimbazi wametakiwa kuwa watulivu kwamba kila mtu anayestahili atalipwa fidia yake.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Miradi ya DMDP pamoja na Mradi wa Kuendeleza Bonde la Mto Msimbazi Mhandisi Humphrey Kanyenye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi baada ya kuibuka kwa baadhi ya wakazi hao kulalamika kwamba fidia ni ndogo.

Mhandisi Kanyeye amesema kuwa Serikali haipo tayari kumdhulumu mtu yeyote haki yake, hivyo kama kuna mtu mwenye malalamiko anatakiwa kuyaripoti kwenye dawati la malalamiko ili yafanyiwe kazi.

“Kama kuna malalamiko yapelekwe kwenye dawati la malalamiko na utasikilizwa, na kama hutaridhika nenda mahakamani, lakini kulalamika kiholela ni kuleta taharuki,” amesema Mhandisi Kanyeye.

Amebainisha kuwa kwa sasa wanaendelea na uhakiki wa thamani zinazoathirika na mradi huo ili kujua gharama ya fidia ambayo kila mtu anastahili kulipwa.

Kwamba katika zoezi hilo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wamashafanyiwa uthamini wa mali zao na wamekubaliana na fidia walizowekewa na wapo wachache waliokataa, lakini wanaendelea kushughulikia jambo hilo.

“Kimsingi walitakiwa wasilipwe kwani walishapewa notisi tangu mwaka 1979 kwasababu eneo hilo ni hatarishi, lakini Serikali kwa kujali imeamua walipwe, hata hivyo hatuwezi kulipa kitu ambacho hakipo,” amebainsha Mhandisi Kanyenye.

Mhandisi Kanyeye amesisitiza kuwa wanalipa thamani ya mali iliyopo kwa sasa na sio vinginevyo na kueleza kuwa wao baadhi ya wananchi wenye matarajio makubwa kuliko uhalisia.


No comments:

Post a Comment

Pages