Na John Richard Marwa
Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC msimu huu Yanga SC wamejipanga vilivyo kwenda kumalizia shughuli ya hatua ya makundi mjini Lubumbashi jumapili hii.
Yanga watashuka dimbani kusaka nafasi ya kuongoza kundi D la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC ambapo kama watashinda kwa idadi kubwa ya mabao wataweza kuongoza kundi lao dhidi ya US Monastiry ambao nao watakuwa nyumbani wanakidimua na Real Bamako.
Yanga wanaingia wakiwa na pointi 10 sawa na Monastiry wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku kila timu ikihitaji kufanya vizuri zaidi katika michezo hiyo ya mwisho kwa kushinda kwa mabao mengi zaidi ili kuongeza kundi lao.
No comments:
Post a Comment