HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2023

Nabii Oliva asema Kanisa la Mungu linahitaji matengenezo makubwa, aungana na wenzake kupinga vitendo vya unyanyasaji na ushoga

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Mtunza Fedha wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania, Nabii Dkt Oliva Elisha  (pichani) amesema Kanisa la Mungu linahitaji matengenezo makubwa hivyo watumishi wote ambao wameitwa na Mungu wanapaswa kusoma na kusikiliza maelezo ya watumishi wengine waliowatangulia kama Mahaba wa Kiroho.


 

Nabii Dkt Olivia ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kando ya kongamano la umoja wa mitume na manabii lililolenga kumshukuru Mungu kwa mambo mbalimbali sambamba na kuangazia mafanikio ya miaka miwili ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani ambalo limepewa jina la “Kongamano la Mshangilio”.

Amesema kuwa watumishi wa Mungu endapo watasikilizana na kuwa na umoja thabiti hatua hiyo itapelekea pia kuwa na mashirikiano mema na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii nchini.

Ameongeza kuwa wao kama mitume na manabii watasimama kwa imani na kwa pamoja kumdai Mungu watanzania wote wawe salama na kuliepusha Taifa na mmomonyoko mkubwa wa maadili uliopo kwa sasa ambao umechangia kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto sambamba na vitendo vya ulawiti na ushoga hivyo watashirikiana vyema na serikali kutokomeza vitendo hivyo.

Aidha Nabii Dkt Olivia pia amewataka watanzania kuungana kwa pamoja na Rais Dkt Samia katika kupiga vita rushwa,ufisadi na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ili kuendelea kuitunza amani ya nchi ambayo inaanzia katika ngazi ya familia.

“mimi kama mtumishi wa Mungu kijana,nawaasa vijana kuwa Mungu anaweza kumtumia kijana kwani kijana anaweza kufanya kazi akatengeneza uchumi,akatoka kwenye mambo ya tamaa za kimwili hivyo vijana tufanye kazi kwa bidii”alisisitiza nabii Dkt. Oliva Elisha 

Hata hivyo amewasihi mitume na manabii hapa nchini kujisajili na umoja huo ili kuendelea kupeleka neno la Mungu kwa watanzania na dunia kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages