HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2023

AZIZ KI AJIBU KWA VITENDO, MAYELE, MORRISON WAISASAMBUA KAGERA SUGAR

Na John Richard Marwa


Kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso na klabu ya Yanga Stephen Aziz Ki amejibu kwa vitendo waliokuwa wakimbeza kiwango chake cha hivi karibuni kwa kufunga mabao matatu akiongoza Yanga katika ushindi wa mabao (5-0) dhidi ya Kagera Sugar.

Ni mchezo wa mzunguko wa 25 kwa Mabingwa watetezi Young Africans msimu huu wakijikusanyia pointi 68 kileleni mwa msimamo wa NBC PL wakihitaji ushindi katika michezo mitatu tu kati ya mitanao iliyosalia kutawazwa Mabingwa msimu huu wa 2022/23.


Yanga walihitaji ushindi wa leo dhidi ya Kagera kujiweka sawa katika mbio za kutetea ubingwa wao, wakifahamu kama wangepoteza mchezo huo ingekuwa rahisi kwa watani zao Simba kuendelea kuweka matumaini hai ya kuusaka uchampioni msimu huu.


Mabao mengine ya Yanga yamewekwa kimiani na Fiston Mayele na Bernard Morrison na kukamilisha 5G jioni ya leo.


Ushindi huo kwa Yanga unawafanya kuingia kwenye Derby April 16 dhidi ya watani zao Simba SC katika Dimba la Benjamin Mkapa mchezo unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.


Wakati Yanga wakijikita kileleni mwa msimamo wa NBC PL, mshambuliaji wao kinara Fiston Mayele amezidi kujiimarisha katika mbio za utafutaji kiatu cha ufungaji bora msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Pages