HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2023

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu kufanyika Dar

Kufuatia kuwepo kwa mkutano huo nchini Tanzania Leo tarehe 15 Juni 2023 katika Ukumbi wa Karibu Art Gallery jijini Dar Es Salaam Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Kedmon Mapana amekutana na baadhi ya wanakamati kutoka Makao Makuu ya Benki ya Dunia nchini Marekani wakiongozwa na Bi. Salina Giri ambapo lengo kuu likiwa ni maandalizi ya mkutano huo.

Aidha katika Kikao hicho pia walijadiliana ni kwa jinsi gani Baraza la Sanaa la Taifa kwa kushirikiana na Wadau wengine wa Sanaa kama vile Nafasi Art Space wanaweza kutumia mkutano huo kuwapatia wanasii fursa ya kuonesha na kuuza kazi zao za Sanaa kwa wageni na kufungua milango ya kibiashara.


Dkt. Mapana aliongeza kusema kuwa, kamati kutoka Wizara ya Fedha Tanzania na Benki ya Duniani ambayo imefika kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi kutoka Afrika utakaofanyika tarehe 25-26 Julai 2023 jijini Dar Es Salaam wamepewa jukumu pia la kuwaleta Wasanii pamoja na hivyo BASATA kama waratibu na wasimamizi wa Sanaa Tanzania imechukua jukumu la kukutana nao na kuwaonesha baadhi ya kazi za Sanaa zinazopatikana hapa nchini ambapo wamepata nafasi ya kutembelea kituo cha Sanaa Cha Karibu Art Gallery  jijini Dar Es Salaam pamoja na kijiji Cha Sanaa Cha Mwenge Ili waweze kuona Sanaa zipi zitafaa kutumika katika mkutano huo,

Dkt Mapana ambaye aliambatana na Raisi wa TAFCA,Bw.Adrian Nyangamale amewahakikishia kuwa, BASATA kupitia Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo itatota ushikiano wa kutosha kufanikisha zoezi likwenda kama ilivyopangwa.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Karibu Art Gallery,Bw.Origenes Uiso amelishukuru Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Wizara ya Fedha pamoja na Benki ya Dunia kutoka Makao Makuu Washington DC nchini Marekani kwa kutembelea Karibu Art Gallery na kwamba Menejimenti ya Karibu Art Gallery itatumia fursa hiyo kuitangaza Sanaa ya Tanzania kibiashara lakini pia kutoa elimu juu ya Sanaa ya Tanzania kwa wageni kupitia fani ya uchongaji, Uchoraji,ususi ,ufinyanzi nk.

No comments:

Post a Comment

Pages