HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga achangia ujenzi nyumba za watumishi wa chama

 Na Mashaka Mhando Tanga


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajabu Abdalahman Abdalah MNEC, ametoa tofari 54,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za watumishi wa chama katika wilaya zote za mkoa wa Tanga.



Mwenyekiti huyo alliahidi kutoa tofari hizo baada ya kukagua kiwanja cha CCM kilichopo wilayani Handeni na kumwagiza Katibu wa CCM mkoa wa Tanga Suleiman Mzee Suleiman kuhakikisha kila wilaya inavyo viwanja vyake vyenye hati.


Alisema katika kipindi  cha uongozi wake, atahakikisha anasimamia ujenzi huo na kwakusisitiza hilo, aliahidi kutoa tofari hizo kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa nyumba hizo uanze mara moja.


Alisema kila wilaya mkoani hapa, atahakikisha zinajengwa nyumba nne za watumishi hao ambao ni Katibu wa wilaya na makatibu wa jumuiya za Vijana, UWT na Wazazi.


"Katibu hakikisha kila wilaya tayari wamekuwa na viwanja kama hiki cha hapa Handeni, nataka kipindi changu niwe nimesimamia ujenzi wa nyumba za watumishi wa chama," alisema Mwenyekiti huyo.


Akiwa wilayani Kilindi Mwenyekiti huyo alitoa kiasi cha sh. 680,000 kwa ajili ya kununulia bati 40 zitakaezekea jengo la ofisi ya CCM kata ya Tunguli.


Tayari jengo hilo limefikia hatua ya boma na Mwenyekiti ameaahidi kurudi Juni 23 mwaka huu kutazama matumizi ya fedha hizo.


Pia mwenyekiti huyo alitoa kiasi cha sh. 4,800,000 kwa ajili ya kumalizia hatua za mwisho za ofisi ya CCM wilayani Kilindi baada ya Katibu wa CCM wilaya hiyo Suraiya Kangusu kumwambia zinahitajika fedha hizo ili ofisi hiyo ikamilike. Mwenyekiti alitoa fedha hizo papo hapo.


Akizungumza katika maeneo hayo Katibu wa CCM mkoa Suleiman Mzee Suleiman aliahidi kukufanyia kazi ujenzi wa nyumba hizo.


Mwenyekiti alifanya ziara ya kutembelea wilaya za Kilindi, Handeni, Pangani na Tanga mjini. Ziara nyingine ya kumalizia wilaya zilizobaki Mwenyekiti ataanza tena Julai 5 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages