HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 14, 2023

Rais Samia azungumza na Viongozi pamoja na Machifu katika Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika Kisesa Mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Machifu wakati alipohudhuria Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

Mtoto Goziberti Bwele (14) wa kikundi cha Ngoma za Asili ca Utandawazi Theater Group (Matwigachallo) kutoka Ukerewe akionesha umahiri wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza mtoto  Goziberti Bwele (14) wa kikundi cha Ngoma za Asili cha Utandawazi Theater Group (Matwigachallo)  kutoka Ukerewe kutokana na umahiri wake wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023. Tamasha la Bulabo huleta pamoja shughuli za Utamaduni na zile za dini.

Vikundi mbalimbali vya ngoma za asili kutoka maeneo ya Usukumani, ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu vikitumbuiza katika Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.


 
 Shamrashamra za Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

No comments:

Post a Comment

Pages