Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupata Hati Safi Mara Saba mfululizo (Unqualified Audit Opinion) katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo jijini humo katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatouglou wakati wa Baraza Maalum la Madiwani kupokea na kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2022.
Pamoja na pongezi hizo, Mhe.Chalamila ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuzuia hoja za ukaguzi, pamoja na kuhakikisha inaweka mfumo Madhubuti wa kusimamia mashine za ukusanyaji wa mapato (POS).
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Omary Kumbilamoto amesema “Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hufanyika kila Mwaka baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, na Kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sura ya 418 na kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na Kamati za Kudumu za Bunge hivyo nipende kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupata hati safi miaka saba mfululizo huku akimuhakikishia mkuu wa mkoa huo kutekeleza yote aliyoyaagiza."
Aidha Bararaza la Madiwani liliweza kupokea na kupitisha taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment