HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2023

Upendo Wella ataka ushirikiano Same

Na Mwandishi Wetu, Same

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amewaomba viongozi, watumishi wa umma, binafsi na wananchi wilayani humo  kuendeleza ushirikiano na  uwajibikaji ili kufanikisha adhma ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kuleta maendeleo.

Wella ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Sospeter Magonera aliyehamishiwa Wilaya ya Hai mkoa humo katika mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Rais Samia.

Katibu huyo alisema ushirikiano kwenye utendaji ndio njia pekee na rahisi kwa kila mmoja kufanikisha wajibu wake, hivyo atasikitika kuona baadhi ya watoaji wa umma wanakuwa chanzo cha kudorora.

"Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia wananchi wa Same hasa kutatua migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na wote tuwe kitu kimoja, ili  tuendelee kukuza uchumi wa Taifa letu," alisema Wella.

Kwa upande wake Katibu Tawala aliyehamishwa, Magonera amewashukuru watumishi na wakazi wote wa Same kwa ushirikiano katika kipindi chote cha utumushi wake kwenye wilaya hiyo, akisema kwa kua lengo la Serikali ni kujenga nchi na kuleta maendeleo, ushirikiano ndio msingi wa kufanikisha mipango hiyo.

"Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu nyie watumishi na wananchi kwani mmenifanya nifanye kazi yangu katika mazingira mazuri, naomba muendelee na moyo huo, ili dhamira ya Rais Samia kuwaletea maendeleo iweze kutekelezeka,"alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages