HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2023

Wabunifu ‘Imbeju’ waimwagia Maua Benki ya CRDB

Mkurugenzi Mkuu Tume ya TEHAMA, Dk. Nkundwe Mwasaga, akitoa mada Dar es Salaam Juni 22, 2023 kwa baadhi ya wabunifu waliochaguliwa kwenye Programu ya Benki ya CRDB ya Imbeju inayolenga kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake.

Afisa Usajili Brela, Englibert Barnabas.
 
Afisa Leseni Mkuu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Abas Cothema, akitoa mada kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu usajili wa kampuni na biashara.

Msaidizi wa Usajili Mwandamizi Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Nassoro Mtavu, akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo ya Programu ya Benki ya CRDB ya Imbeju inayolenga kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake. 

 

Meneja Usajili Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA), Philemon Kilaka, akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo ya Programu ya Benki ya CRDB ya Imbeju inayolenga kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake. 



 

 

NA MWANDISHI WETU

 

 

WABUNIFU wa Programu ya Imbeju iliyoandaliwa na benki ya CRDB yenye lengo la kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake wameimwagia maua Benki hiyo kwa mafunzo hayo ambayo yanataraji kufika tamati hapo kesho jijini  Dar es Salaam.

 

Washiriki hao ni kati ya wabunifu 709 waliotuma maombi yao kuanzia Machi 12 Program hiyo ilipozinduliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) na kukidhi vigezo vya awali vilivyowekwa.

 

 

Wamesema mafunzo hayo yamewaimarisha kifikra na kimtazamo na sasa wanayonafasi ya kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja, taasisi na taifa kwa ujumla.

 

Fatma Sulyman mshiriki wa program hiyo amesema program hiyo imewafungua  kujua taratibu za kufuata ili kuweza kufungua biashara na kampuni, pamoja na kujua namna taasisi zinazosimamia haki za biashara na kampuni kama Brela, Cosota na TSA.

 

“Programu hii imetufungua kujua taratibu zipi za kufuata ili kuweza kufungua biashara ama kampuni, ikiwemo kujua taratibu kutoka kwa taasisi ambazo zinatoa haki na kulinda bunifu za biashara ama kampuni.

 

“Kwenye kila ubunifu nimejifunza lazima kuwepo na njia ya kurahisisha utendaji wa kazi yako ili iweze kuwa na ulinzi kutoka kwenye taasisi ambazo zimepewa mamlaka kisheria kusimamia.

 

“Kupitia Programu hii nimejikuta nazalisha mawazo mapya ya ubunifu kutokana na mjumuiko wa washiriki tuliokutana hapa kwani kila mmoja anakuwa na wazo lake ambalo linakuongezea mapana ya ubunifu.” Amesema Fatma.

 

Fatma amewapongeza waandaji wa program ya Imbeju huku akitoa wito kwao kuandaa utaratibu ambao utawezesha jamii ama makundi lengwa kuweza kupata elimu hiyo ili kuweza kutanua wigo wa maarifu  juu ya kufanya kazi na taasisi ambazo ziko kwa ajili ya kusimamia biashara na makampuni pamoja na kazi za Sanaa na ubunifu.

 

Nae Casto Cosmas mshiriki wa Programu hiyo amesema program imekuwa nuzri, manufaa  ni makubwa kwani imewakutanisha na wadau wengi kutoka Nyanja tofauti tofauti.

 

“Programu imekuwa nzuri sana, manufaa ni makubwa sana kwani imetukutanisha na watu mbalimbali kama TSA, COSOTA na BRELA ambao wametupatia uwezo na mafunzo ya kufanikiwa zaidi.

 

“Kipekee niwapongeze waandaaji wa Ibenju kwa fursa hii adhimu kwetu. Wasiishie hapa waendelee kutoa fursa hizi kwa watu  na makundi mbalimbali kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

 

 

Wakati wakitoa maoni hayo leo ni siku ya nne ambapo wamepata mafunzo kutoka kwa Meneja Usajili Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA), Philemon Kilaka,  ambapo amesema haki miliki za ubunifu sio swala la muungano.

 

“Haki miliki ubunifu sio swala la muungano kwa maana Tanzania Bara tuna sheria zetu na Zanzibar wana sheria zao, tuna COSOTA na wao wana COSOTA yao”

 

“Hakimiliki ubunifu hii ni haki ambayo imapa mbunifu haki ya kumiliki kazi yake kwa muda mrefu. Kwa mfano mbunifu wa kitabu anapewa umiliki wa muda wota ambao yuko hai, akisha fariki kazi yake inapewa ulinzi wa miaka 50 kwa familia yake kunufaika na baada ya hapo umiliki unarudi kwa jamii.” Amesema Kilaka.

 

Kwa upande  wa Msaidizi wa Usajili Mwandamizi Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Nassoro Mtavu amesema Alama ya bidhaa na huduma ni alama pekee ambayo inatambulisha bidhaa sokoni.

 

“Alama ya bidhaa na huduma ni alama pekee ambayo inatambulisha bidhaa sokoni. Kwa mfano, mtu akienda dukani anahitaji maji lazima ataje jina la aina ya maji anayohitaji, kama Uhai au Kilimanjaro kwa sababu ndio alama ya nembo ya bidhaa anayoihitaji.

 

Amesema “unapotaka kutuma maombi kwa msajili lazima uzingatie jina la biashara na nembo ya bidhaa ama huduma unayoipeleka sokoni na daraja lake. Nembo ya bidhaa ama huduma ambayo ni maarufu sokoni ina ulinzi wa moja kwa moja kutoka Brela.” Amesema Mtavu

 

Mafunzo  ya Programu ya Benki ya CRDB ya Imbeju inayolenga kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake kwa awamu ya kwanza yanatarji kufika tamati hapo kesho ambapo washiriki watapatiwa vyeti vya ushiriki kabla ya kuingia awamu wa pili ya program ya Ibenju.

No comments:

Post a Comment

Pages