HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2023

Wazee, viongozi wa Dini Muheza waombwa kushirikiana katika kuleta maendeleo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dk. Jumaa Mhina.

 

Na Mashaka Mhando, Muheza

 

WAZEE na viongozi wa dini, wilayani Muheza wameombwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya hiyo katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana na wazee pamoja na viongozi wa dini,
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Dk. Jumaa Mhina alisema wazee ni tunu ya Taifa ambao hawapaswi kubaki nyuma katika maendeleo.

Aidha Mkurugenzi huyo pia amewaomba Wazee na viongozi hao wa dini kusaidia Serikali katika kukemea vitendo vya Ukatili unaotaka kuota mizizi kwenye Jamii.

Dk. Mhina alikutana na wazee hao ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha mara baada ya kuhamishiwa Wilayani hapo kufuatia mabadiliko  yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Dk, Samia Sulluh Hassan kwa Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa Wilaya mbalimbali .

Alisema taarifa ambazo amepatiwa zinaonyesha Halmashauri ya Muheza imekuwa na Matukio ya Vitendo vya Ukatili wa Kingono na wakijinsia na amewaomba kutumia nafasi walizo nazo kwenye Jamii katika kukemea vitendo hivyo.

Pia Mkurugenzi Mtendaji ametumia kikao hicho kuwaomba Wazee na Viongozi wa dini kusaidia kuhamasisha Wananchi wa Muheza kushiriki kwenye ujenzi wa Miradi ya Maendeleo.

Alisema wananchi wanaposhiriki kwenye Misaragambo na hata kuchangia michango ya hiyali itasaidia kukamilisha miradi kwa wakati jambi litakaloleta faida ya Wanajamii wa Muheza katika kupata huduma mbalimbali.

Aidha Mkurugenzi Dk. Mhina amesema Wazee ni tunu muhimu kwa Taifa la Tanzania na amewahakikishia kwamba Halmashauri inakwenda kusimamia Changamoto za huduma za Afya wanazopaswa kupata bure kwakuwa anafahamu  changamoto ambazo wanakutana nazo kwenye zahanati na vituo vya afya .

"Mimi naomba tushirikiane kutekeleza malengo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan haiko nyuma ina program ya kusaidia wazee kwa kuwapatia Vitambulisho vya matibabu bure"

Hivyo ameongeza kwakusema kukamilika kwa Hospitali ya Wilaya ndio kutamaliza changamoto za Wazee, Wakinamama na Watoto ambapo tayari Rais Dkt. Samia ameshatoa fedha kwajili ya kukamilisha Ujenzi.

Kwaupande wao Wazee na viongozi wa dini ambao wamehudhuria kikao hicho licha ya kubainisha changamoto wamemuhakikishia kumpatia ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha anatimiza Majukumu ya kumsaidia Rais katika kuwatumikia Wananchi wa Wilaya hiyo kwa kwenda kutumia nafasi zao kwenye jamii kuyasemea ambayo ameyaomba.

No comments:

Post a Comment

Pages