HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2023

Waletee ‘TVNL’ mambo yameiva

NA JOHN MARWA

HATIMAYE Kocha Mkuu Timu za Taifa kwa Mpira wa Wavu Tanzania amewekwa hadharani tayari kwa maandalizi ya kujiwinda na michuano ya Kimataifa mwezi Agosti mwaka huu.

Akimtambulisha Kocha huyo, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Engener Magoti Mtani amesema wamezingatia vigezo vingi kumpata Kocha huyo.

Zoezi hilo limefanyika leo jijini Dar Es Salaam katika Viwanja vya Gwambina ambapo kocha huyo tayari ameshaanza kazi kwa ajili ya kukusanya vipaji kupitia mashindano mbalimbali.
“Kwa kipekee kabisa naomba kumtambulisha kwenu Kocha wa timu za Taifa ambaye ndiye atakuwa Kocha Mkuu na yeye ndiye atashughulika na masuala yote ya kiufundi katika suala la timu zote za Taifa akisaidiana na kamati ya Chama lakini pamoja na Makocha wasaidizi ambao baadae tutakuja kuwataja kila mmoja kwa nafasi yake.

“Karibu sana Kocha Alfred Selengia, huyu ni kocha mwenye cheti cha kimataifa cha Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani (FIVB), kwaiyo tunamtegemea kwa sababu pia ni mtanzania basi swala la uzalendo tunaamini limezingatiwa katika hili, tunategemea kwa kushirikiana naye tunaweza kupata mafanikio makubwa kama Taifa.

“Baada ya muda mrefu tumekuwa na mapumziko ya ratiba za kimataifa kwa timu zetu za Taifa, lakini kwa mwaka huu katika kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani (FIVB) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Wavu Afrika (CAVB), ni mwaka kwa ajili ya michuano ya Timu za Taifa.

“Kwa sababu ni mwaka kwa ajili ya michuano kwa ajili ya Timu za Taifa na sisi kama Taifa hutujabaki nyuma,tunakwenda kushiriki michuano ya Afrika ambayo kwa Wanawake itafanyika Cameroon mwezi wa nane lakini kwa Wanaume itafanyika Cairo Misri mwazi huo huo wa nane.

“Kwa sababu hiyo tumekwisha anza maandalizi ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kupeleka ushindani na sio kwenda kushiriki, kwa hatua za awali kabisa na kwa niaba ya kamati ya maandalizi  ya timu za Taifa.

Baada ya kutambulishwa Kocha Selengia amesema Imani ambayo TAVA wameweka kwake haitaenda bure hivyo atahakikisha anafanya kazi kwa weledi mkubwa.
 
“Binafsi nashukuru kwa Imani kubwa ambayo nimeipata kutoka kwa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania na kupewa  jukumu hili kwa ajili ya kuziandaa Timu zetu za Taifa kwa Wanawake na Wanaume.

“Nina Imani kubwa kwa jukumu hili nitakwenda kulitekeleza vizuri kwa kushiriakiana na kamati, vilevile na benchi la ufundi. Lakini pia nina Imani kubwa sana, wachezaji ambao tuko nao sasa hivi, tuna vijana ambao wako vizuri sana, walioko hapa ndani, vilevile wale ambao wako nje wanacheza Ligi za kimataifa.

“Kwa kuzingatia hayo yote tunaamini kwamba, kwa muda ambao tutakuwa nao wa maandalizi timu zetu zitaandaliwa vizuri na nina Imani tutaenda kufanya kadri ya uwezo wetu.


No comments:

Post a Comment

Pages