HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2023

Ligi Kuu U-20 yashika kasi Chamazi


NA JOHN MARWA


KASI ya Ligi kuu ya vijana chini ya miaka 20 imeshika hatamu baada ya kuzinduliwa hapo jana kwa michezo minne kupigwa ya Kundi A na C huku leo michezo mingine minne ya kundi B na D kulindima.


Ligi hiyo inashirikisha klabu 16 ambazo ndio zilishiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu uliomalizika. Huku Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo ni Mtibwa Sugar.


Mchezo wa uzinduzi ulizikutanisha Ruvu Shooting dhidi ya Namungo FC majira ya saa nane mchana ambapo Ruvu Shooting waliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Michezo mingine iliyopigwa jana ni Mtibwa Sugar vs Mbeya City, Geita Gold vs KMC FC na Coastal Union vs Singida BS.

 

Leo inatarajiwa kupigwa mitanange mingine minne ambapo Simba SC vs Kagera Sugar, Azam FC vs Ihefu, Polisi Tanzania vs Tanzania Prisons na Yanga SC vs Dodoma Jiji. Michezo yote kwa timu zote inapigwa katika Dimba la Azam Complex.

 

Msimu huu wa ligi ya vijana unatarajia kufika tamati julai 2 mwaka huu ambapo ndio siku ya fainali ya kumpata Bingwa mpya wa msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Pages