HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2023

EPZA YAONESHA FURSA KATIKA SEKTA YA KILIMO KWA KUYAONGEZEA THAMANI MAZAO

Na Magrethy Katengu

Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje EPZA imekuwa Mstari wa mbele kuwaonesha fursa Wakulima kwa kuongeza mazao yao katika mnyororo wa thamani kupitia viwanda vikubwa, kati,na vidogo ili bidhaa zao zinazodhalishwa ziweze kuuzika kimataifa .

Akizungumza Jijini Dar es salaam Afisa Mhamasishaji Uwekezaji   EPZA Nakadongo Fares   amesema wao wamekuwa wakitoa leseni kwa viwanda vinavyozalisha kwa kuchukua malighafi ikiwemo kiwanda walochonacho cha Tiba lishe kuchukua mimea na kuvichakata kisha kusafirisha kwenda kuuza nje ya nchi

Hata hivyo amesema kiwanda hiko cha Tiba lishe kipo Bagamoyo kimekuwa kinawasaidia wananchi kwa kuwapatia mafunzo na kuchukua mimea yao na kuitengeneza kuiongezea thamani hivyo wananchi walipata fursa ya kujifunza teknolojia ya kisasa namna bora ya kulima

"Hii ni fursa kubwa kupitia mwekezaji anayetaka kuwekeza kupitia kilimo kwani kuwepo kwa kiwanda hiki cha Tiba lishe kinatengezena fusa nyingi Nchi inapata kunakuwa na mnyororo kuanzia kwa wakulima kupata mafunzo kulima kilimo cha Organiki pasipo kuweka kemikali yeyote katika mimea mbalimbali ambayo waliwafundisha kisha kununua kutoka kwao na kuzalisha kisha kusafirisha kupeleka nje ya nchi"amesema Fares

Sanjari na hayo amesema Elimu ya teknolojia mpya  liyokuwa ikotolewa inakwenda kwa wazawa wakulima na imewasaidia wenyewe kuboresha kulima kisasa zaidi kupitia teknolojia waliyoipata kwa  kuboresha bidhaa zao baadae kusimama wenyewe kupitia kumiliki viwanda vidogo na vya kati kuzalisha bidhaa zap wenyewe kwenda nje ya nchi.

"Nasisi Watanzania kupitia Wawekezaji hao tunapata fedha za kigeni kupitia viwanda kuuza bidhaa nje ya nchi na inasaidia kupunguza uingizwaji bidhaa za nje badala yake na sisi tunatoa kwenda kuuza na kutusaidia kujenga uchimi imara "amesema Fares

Aidha amesema EPZA ina  Mfumo kiganjani  wa kuhudumia Mto popote alipo pasipo kusafiri kwenda Ofisini kwa kila kitu wanafanya kupitia mtandao na wameweka mfumo huo ili kurahisisha uwekezaji na kujua fursa mabalimbali hivyo Wananchi mnakaribishwa kuja Banda la Sabasaba kupata elimu


 Sambamba na hayo wamekuwa mstari wa mbele wakiwapatia elimu baadhi ya viongozi wa  Mikoa ikiwemo Kigoma ,Mbeya kuhusu fursa zinazopatikana Mamlaka hiyo na kuwahamasisha kuandaa maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia  uwekezaji wa viwanda ambavyo vitasaidia kuongeza thamani mazao yao kwa  kujengea miundombinu ikiwemo barabara


No comments:

Post a Comment

Pages