HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2023

SERIKALI YA ZANZIBARI KUINUA WANANCHI WAKE KUPITIA UCHUMI WA BLUU .

Na Magrethy Katengu

Serikali ya Zanzibar iliyo chini ya Rais Ally Hassan Mwinyi imekuwa ikiongeza jitihada za kusaidia uchumi wa bluu wa Bahari usaidie wananchi wake huausani wavuvi kwa kuwatengea maeneo maalumu ili wasinyanyasike ikiwemo eneo la Kama, Unguja na Pemba.



Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Msimamizi Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) Ameir Mshenga na Waandishi wa habari katika mahojiano maalumu katika Banda lao amesema watu wanafanya kazi za dagaa kipato chao ni changamoto hivyo kupitia sera ya uchumi wa bluu wamekuwa wakiwekewa mazingira wezeshi ili wafanye shughuli zao na kukuza vipato vyao huku wakilipa kodi ya serikali ili kusaidia miradi ya kiserikali itekelezwe.

"Kupitia Uchumi wa Bluu Kampuni hii inafanya kazi kubwa na imeaminika na ina miradi  mitano mikubwa katika nchi ya Tanzania na Zanzibari kupitia sekta ya dagaa hivyo kupitia sera ya Zanzibar kuhakikisha wanamkomboa mtu ambaye alikuwa anadharaulika kutokana na kipato chake lakini kwa sasa anathaminika kwa kupewa. mikopo mbalimbali"amesema .

Sambamba na hayo amesema Shughuli ya dagaa imekuwa ikichukua  watu wengi Tanzania na Zanzibari na Rais Mwinyi kwa kutambua hilo ametenga kiasi cha  fedha bilioni 34 kwa ajili ya kutengeneza Mradi mkubwa wa dagaa ambao umeshaanza kwa kununu baadhi ya vifaa vya kiteknolojia vya kuvulia dagaa na kuandaa eneo la hekta 19 kwa ajili ya wajasriamali wadogo kufanya shughuli zao zadagaa na kutakuwa na viwanda vya usindikaji dagaa.
.

Hata hivyo amesema kuwa eneo hilo la hekta 19 kutakuwepo na nyumba za wajasriamali wadogo wa dagaa lengo ni kuwainua kiuchumi ili bidhaa yao iwe bora isiyo na mchanga hata iwe inasafirishwa nje ya nchi na wafanyabiashara wakubwa

Aidha Amesema Muamko wa Wajasriamali kufanya shughuli hiyo ni mkubwa kwani kupitia Rais Dk. Mwinyi kutenga fedha na eneo kutapunguza vilio vya baadhi ya watu wanaolalamika kukosa ajira watajiajiri wenyewe .

No comments:

Post a Comment

Pages