HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2023

Kibabage atua Twiga na Jangwani

Na John Marwa


Mlinzi wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Singida Fountain Gate FC Nickson Kibabage ametua mitaa ya Twiga na Jangwani kw kandarasa ya misimu mitatu.



Kibabage ametambulishwa usiku mnene kuungana na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ikiwa ni kuongeza Nguvu katika kukisuka kikosi kwa ajili ya msimu ujao.


Mlinzi huyo mahiri anaungana na nyota wenzake ambao walikuwa wote katika kikosi cha Mtibwa Sugar, Abutwalibu Mshery, Shomary Kibwana na Dickson Job.


Kibabage anaungana na kikosi cha Wana Jangwani katika safari yao ya kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi Nyasa Big Bullets hapo kesho katika siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Taifa hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages