HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2023

Nyie hamuogopi?! Alassane Diao atua na mabao Chamazi



Na John Marwa 

Shambuliaji la kutosha linalo pachika mabao ya kila aina anetambulishwa kujiunga na Azam FC ikiwa ni muendelezo wa kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao wa 2023/24


Azam imemtanbulisha Diao raia wa Senegal akichukua nafasi ya Rogers Kola ambaye ameachana na waoka mikate Azam.


"Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji hatari my kutoka Senegal, Alassane Diao, akitokea US Goree." Imeeleza taarifa hiyo.

Diao anaungana na wa Senegal Cheikh Tidiane Sidibe (mlinzi), Kocha Mkuu, Youssouph Dabo, Kocha wa Makipa, Khalifa Ababakar Fall, na Mtaalamu wa uchambuzi wa mechi Ibrahim Diop.

No comments:

Post a Comment

Pages