HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2023

Shaka: Rais Samia kioo cha uongozi Afrika

*Asema anayoyafanya anatafsiri kwa vitendo njia za wapigania ukombozi Afrika.

*Ataka wananchi, viongozi wa majukwaa mbalimbali na mashirika yamuunge mkono

Na Mwandishi  Wetu, Kilosa Morogoro

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kioo kipya cha uongozi Tanzania na Afrika kwa sasa, ambaye anafuata nyayo za waasisi wa Umoja wa Afrika katika kuleta umoja na mshikamano kwa Watanzania ili kuwaletea manufaa, ustawi na maendeleo.



Shaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, ameyamesema jana  katika viwanja wa Magubike wilayani Kilosa, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Magubike.

Amesema  waanzilishi hao, wakiwemo Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani  Karume (Tanzania) Kwame Nkurumah (Ghana), Jomo Kenyata (Kenya), Gamal Abdi Naaser (Misri), na Ahmed Sekeu Toure (Guinea ) ni vioo vya uongozi unaopaswa kuigwa.

"Wazee hawa walifanya kazi kubwa katika kuimarisha umoja na upendo kwenye nchi zao na afrika kwa ujumla. Waliyafanya hayo  kwa uadilifu, uaminifu na kujitolea wakati wote. Na Rais Samia amekuwa akupita kwenye njia hiyo
hiyo kwa kivitendo,” amesema Shaka.

Amesema serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia  inapambana kuimarisha maisha ya watanzania, kuhimiza usawa na haki, kutanua wigo wa demokrasia na ushirikishwaji wananchi kwa kuwataka wajitume zaidi hususan kuzalisha mali.

"Wahenga wetu wana msemo usemao kioo cha mtu ni mtu,  kila mmoja ajipime, ajitathmini na kujitambua kutokana na usahihi wa mwenzake. Aina ya uongozi wa Dk Samia ndiyo unaohitajika katika kuwatumikia wanyonge na masikini walioko barani Afrika," amesema Shaka.

Hata hivyo, amesema nchi za Afrika zilitaka  ziwe huru na kujitawala, uhuru huo  hautakuwa na maana iwapo haitawekwa mikakati thabiti ya kuboresha matumizi ya rasilimali za nchi ili zisaidie kukuza uchumi kwa dhamira ya kuleta maendeleo endelevu kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Shaka amewataka wananchi, viongozi wa kisiasa, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, madhehebu ya dini na makundi mengine ya kijamii kusimama imara kuunga mkono juhudi za serikali ya Dk Samia katika mapambano ya kuwaletea kuimarisha uchumi kuweza kuharakisha maendeleo ya watanzania.



No comments:

Post a Comment

Pages