HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2023

Muarobaini wakudhibiti tembo vamizi waja

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amezindua programu  maalum ya ujenzi wa vituo maalum 16 kwa ajili ya kuthibiti wanyama waharibifu  akiwemo tembo katika maeneo mbalimbali nchini. Vituo hivyo vinatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi  bilioni 1.



Mchengerwa amesema hayo wakati akizindua program hiyo na kushiriki  ujenzi wa kituo cha kudhibiti wanyama waharibifu katika Kijiji cha Muheza wilayani Same mkoani Kilimanjaro.           

Amefafanua kuwa program hiyo ni mkakati maalum ambao utasaidia kukabiliana na wimbi la wanyama waharibifu hususan tembo ambao wameongezeka kwa kiasi kikubwa  katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na kuimarika kwa uhifadhi.

Amesema Wizara itapeleka askari wa kutosha wa uhifadhi kwenye kila kituo ambao watatakiwa kushirikiana na wananchi kwenye maeneo husika  kuwakabili wanyama hao pindi wanapotokea kwenye makazi ya wananchi na kuwarejesha katika  hifadhi.

Amezitaka taasisi zote zilizochini ya wizara yake kuwa na  ushirikiano mkubwa na wananchi ambapo amewataka kushuka chini kwa wananchi na  kufanya uhifadhi wa raslimali hizo kwa  karibu huku akifafanua kuwa wahifadhi namba moja wa raslimali ni wananchi.

Akifafanua kuhusu program hizo amesema  program hiyo ni mkakati  madhubuti na endelevu wa kuhakikisha kuwa changamoto hiyo inapata ufumbuzi wa kudumu.

Aidha amelielekeza Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) kuhakikisha  linaleta helikopita ndani ya siku mbili katika  eneo la Same kwa ajili ya kuja kusaidia zoezi la kuondoa  makundi ya wanyama tembo walio kwenye  maeneo ya makazi  na kuwarejesha  hifadhini.

"Eneo hili lipo karibu na Hifadhi ya Mkomazi ambayo ina idadi kubwa ya Tembo," alisema.

Waziri Mchengerwa ametaja maeneo nane ya awali yatakayojengwa  vituo hivi kupitia Mamlaka ya Ngorongoro kuwa ni pamoja na Same, Kilosa, Manyoni, Monduli, Korogwe, Babati, Morogoro vijijini na Rufiji

Pia ameiagiza Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kujenga vituo nane  kama  hivi kwenye maeneo mengine yenye changamoto zaidi.

Baadhi ya wakazi wa eneo hili wamepongeza jitihada kubwa inayofanywa  na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki  kupitia ya Wizara  Maliasili na Utalii ambapo wamesema mikakati hiyo  ya itasaidia  kupata  mazao ambayo yamekuwa yakiliwa na tembo mara yanapokomaa.

“Nampongeza Rais Samia kwa kutuletea  vituo hivi ambavyo ni mkombozi wetu kwa kuwa kwa miaka mitatu sasa  tumekuwa  tukishindwa kuvuna mazao yetu kwa sababu ya kuliwa na tembo," amefafanua Juma Khalifa Mkaazi wa eneo hil.

No comments:

Post a Comment

Pages