HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2023

DC Mpogolo amshukuru Rais Dkt. Samia kwa kufanya makubwa Ilala Sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu ya Barabara

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba makubwa anayofanya maendeleo ya Wilaya hiyo katika Sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu ya bararabara.
DC Mpogolo amebainisha hayo leo jijini humo wakati akizungumza katika Kongamano la Wamachinga, Bodaboda na Madereva Bajaj la kumpongeza Rais Dkt. Samia lililofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

“Nitumie nafasi hii kuungana na risala zilizotangulia, kumshukuru Rais Dkt. Samia kipekee kwa Wilaya ya Ilala anavyotupendelea. Tunaamini anatupendelea kuliko Wilaya nyingine za Tanzania,” amesema Mpogolo.

Akizungumzia kuhusu Sekta ya Afya, amesema kwamba kwa sasa vipo vituo vya afya saba ambavyo vinaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali ya wilayani humo ikiwemo Kituo cha Afya cha Ghorofa kinachojengwa Mchikichini.

Kwa upande wa Elimu, DC Mpogolo amebainisha kuwa Rais amewapatia kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi wa madaraaa, lakini pia amesema wameweza kujenga Shule mbili mpya.

Kwamba kwa upande wa barabara kupitia TARURA wameweza kuzikarabati hivyo wana Ilala wana kila sababu ya kumshukuru Rais Dkt. Samia.

Kuhusu wamachinga, bodaboda na madereva bajaji ameahidi kuendelea kuwawekea Mazingira mazuri ya Biashara zao.

No comments:

Post a Comment

Pages