HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2023

MASHINDANO YA POOL NANENANE YAANZA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

 

2.Mratibu wa Mashindano ya Nanenane, Michael Machela(katikati) akipiga makofi pamoja na Wachezaji mbalimbali wanaoshiriki mashindano hayo mara baada ya uzinduzi  uliofanyika katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.

Msanii wa nyimbo za Mashairi na mchezaji wa timu ya Skylight B, Mrisho Mpoto (Mjomba) akicheza dhidi ya timu ya Vegas ya Sinza wakati wa masindano ya nane nane yanayoendelea katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.Vegas ilishinda 13 – 1.

 

Na Mwandishi Wetu

 

MASHINDANO ya wazi  ya mchezo wa Pool ambayo hufanyika kila mwaka katika kipindi cha siku kuu ya nanenane yameaanza rasmi leo katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam yajulikanayo kama “88” Grand Open Pool Competitions 2023.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari Mratibu wa Mashindano hayo na Mwakilishi wa Kampuni ya Watengenezaji wa meza za Pool ya Kenice, Michael Machela alisema mashindano hayo yatachukua siku tatu yakijumuisha timu za Mikoa ,mchezaji mmoja mmoja Wanaume pamoja na Wanawake.

 

Alisema Machela, jumla ya timu 16 zilijiandikisha na tayari zinashiriki mashindano hayo.

 

Machela pia alisema jumla ya wachezaji 128 wamethibitisha kushiriki na tayari wamesharipoti eneo la mashindano ikiwa ni pamoja na Wachezaji kutoka nje ya Nchi.


No comments:

Post a Comment

Pages