HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2023

BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lihakikishe kuwa Mradi wa Baraza hilo ujulikanao kama BASATA Vibes unawafikia Wasanii mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ili azma ya Serikali ya kukuza sanaa nchini itimie.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo leo Septamba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Mradi wa BASATA Vibes na Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa hapa nchini wenye lengo la kuimarisha maonesho ya Sanaa,  kutoa mafunzo kwa Wadau wa Sanaa na kuwajengea uwezo wa kuandaa matukio ya burudani.

" Kupitia Ubalozi wa Ufaransa natumia nafasi hii kwenu Ubalozi kuhakikisha mashindano ya michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024 uhusishe burudani kutoka kwa wasanii wetu, hili naomba mlizingatie sana, pia katika mashindano hayo naomba mhakikishe Watanzania wanapata nafasi za kutosha kwenye michezo hiyo kwakua vigezo vya kushiriki wanavyo" amesisitiza  Mhe. Ndumbaro.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amesema kuwa atahakikisha jukumu alilokabidhiwa na Mhe. Waziri la kuwapata Wanamuziki Wazuri na wenye sifa ya kuburudisha katika mashindano hayo linatimia .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma akizungumza kwa niaba  ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema Sekta hiyo inatoa fursa kwa Wadau wake kupata nafasi katika soko la Kimataifa.

Aidha, Mkurugenzi wa  Kituo hicho Bi. Flora  Valleur amesema mradi huo  pia utahusisha kujifunza Lugha la Kifaransa, na kupata nafasi kwa wasanii wa Tanzania kuhudhuria na kutoa burudani kwenye majukwaa ya burudani ya nchi hiyo


No comments:

Post a Comment

Pages