HABARI MSETO (HEADER)


October 13, 2023

Asilimia 80 ya wagonjwa wa saratani wanachelewa kugundua Na Selemani Msuya

IMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa saratani ya matiti nchini Tanzania wanagundulika ikiwa wamefikia hatua ya tatu na nne, hiyo ikichangiwa na kukosekana kwa programu za uchunguzi wa awali na upatikanaji duni wa matibabu.



Hayo yamesemwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matembezi ya kupambana na saratani yatakayofanyika Oktoba 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Matembezi hayo yameandaliwa na Ubalozi wa Sweden, Shujaa Cancer Foundation, ELEKTA ya Sweden, Hospitali ya Ocean Road na Shirika la Afya Duniani (WHO).


Balozi Ozaki amesema matembezi hayo yanalenga kutoa tahadhari juu ya pendo la huduma za saratani nchini na duniani kwa ujumla.


Amesema tafiti zinaonesha asilimia 80 ya wagonjwa wa saratani ya matiti nchini wanagundulika wakiwa katika hatua ya tatu na nne hali ambayo inasababisha wasipone, hivyo kunahitajika jitihada zaidi kukabiliana na changamoto hiyo.


"Saratani ya matiti Tanzania imeripotiwa kwa kiasi kidogo sana katika miongo miwili iliyopita, isikuwa kwa tafiti chache," amesema.


Balozi Ozaki amesema tatizo hilo linazidi kuwa kubwa kutokana na upatikanaji mdogo wa programu za uchunguzi, utambuzi wa asali na upatikanaji duni wa matibabu kama vile chemotherapy, upasuaji na tiba za mionzi.


Amesema saratani ya matiti ndio saratani ya kawaida zaidi kwa wanawake ulimwenguni na makadirio ya hivi karibuni kuna wagonjwa wapya milioni 2.1 kwa mwaka.


"Saratani ya matiti ndiyo chanzo kikuu cha vifo vinavyohusiana na saratani miongoni mwa wanawake duniani kote, huku zaidi ya vifo 600,000 vinaripotiwa kila mwaka na asilimia 62 vinatokea katika nchi zinazoendelea,"amesema.


Amesema uchaguzi umeonesha kuwa asilimia 6.5 ya wagonjwa wote wa saratani ya matiti nchini ni wanaume ambayo ni zaidi ya mara 10 ya idadi inayoonekana katika sehemu nyingine duniani.


Balozi huyo amesema kampeni ya wiki ya uhamasishaji wa uelewa wa saratani ya matiti mwaka huu ina sambamba na mkakati wa wizara ya afya wa kukabiliana na saratani na kupunguza athari zake kwa jamii, kwa kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa uchaguzi na utambuzi wa mapema.


"Tunayofuraha kuwatangazia kuwa matembezi hayo yatapambwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, "amesema.


Balozi Ozaki amesema iwapo hakutakuwa na jitihada za dhati, Tanzania inatabiriwa kuona ongezeko la asilimia 82 la visa vipya vya saratani ifikapo 2030.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa Shujaa Cancer Foundation, Gloria Mbowe amesema kusudi la matembezi hayo ni kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa kupima saratani ya matiti na kujipima, kusaidia walioathirika, kuangazia umuhimu wa utafiti, kuzuia, matibabu na kupona.


Mbowe amesema pia kuongeza ufahamu wa saratani ya matiti kwa wanaume na wavulana na kuwasaidia wanawake.


"Tunataka watu wajifunze saratani ya matiti sio ugonjwa wa wanawake pekee, wanaume pia huathiriwa, kuonesha mshikamano na usaidizi wa wagonjwa na waathirika wa saratani hiyo, pamoja na wahudumu wa saratani hiyo,"amesema.


Mkurugenzi huyo amesema pia watajifunza kuhusu teknolojia ya kisasa zaidi katika uchaguzi wa saratani nchini iliyofadhiliwa na kampuni ya ELEKTA ya Sweden.


No comments:

Post a Comment

Pages