Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2023 kuhusu kufunguliwa kwa dirisha la Awamu ya Nne ya dirisha la Udahili kwa programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2023/2024.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ithibati, Dkt. Telemu Kassile, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Buyamba Kassaja na Mkuu wa Sehemu ya Uratibu Udahili, Dkt. Francis William.
Na Mwandishi Wetu, Dar
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya Nne ya dirisha la Udahili kwa programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2023/2024.
Kufunguliwa kwa dirisha hilo kunatokana na kukamilika kwa udahili katika awamu zote tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2o23/2024 kukamilika, na majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yatatangazwa na vyuo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo Oktoba 13, 2023 Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuoo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, amesema kuwa tume imepokea maombi ya kuongezwa muda kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.
“Hivyo tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne ya na yamwisho ya inayoanza leo Oktoba 13, 2023 na pia tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa hii vizuri kwa kutuma kwa usahihi maombi yao kwenye vyuo wanavyovipenda. Alisema Prof. Kihampa.
Aidha tume imezielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa Shahada ya Kwanza kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
No comments:
Post a Comment