Serikali
ya Awamu ya Sita imesema itaendelea kudumisha amani na usalama wa Taifa
pomoja kutengeneza mazingira rafiki ya biashara jambo ambalo litasaidia
kuongeza kasi ya wadau wa maendeleo kuja nchini Tanzania kufanya
uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa duka la vifaa vya umeme la
Hisense Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi
na kuifanya kuwa sehemu salama ya kufanya uwekezaji.
Amebainisha
kuwa duka la Hisense litakuwa linauza vifaa vinavyoendana na Teknolojia
ya kisasa jambo ambalo litasaidia kuwa na bidhaa Bora Tanzania
“Hisense
wamekuwa wakiuza bidhaa zenye ubora na gharama nafuu, wakati umefika
kwa Tanzania kuchangia fursa ya kupata bidhaa zenye ubora” amesema
Mpogolo.
Amesisitiza
kuwa Hisense wanatambua Tanzania ni sehemu salama ya kufanya biashara
kutokana mazingira mazuri tafauti na nchi nyengine
Mpogolo
ameongeza kuwa watanzania wanapaswa kuja katika duka la Hisense kwa
ajili ya kujifunza namna ya kutengeneza mazingira mazuri ambayo yanaweza
kushawishi wateja.
“Hisense
ni wafanyabiashara wazuri ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu lao la
kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa” amesema Mhe. Mpogolo.
Kwa
upande wake, Mfanyabiashara Sabaha Said, amesema kuwa kuwa bidhaa za
Hisense inaongoza kwa ubora na teknolojia rafiki kwa matumizi
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment