HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2024

Rais Mwinyi achangia milioni 100 ukarabati Kanisa Katoliki Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha Uhuru wa Kuabudu na kuziagiza taasisi za Kidini kuendelea kuiombea nchi Amani na Umoja.

Rais Dk,Mwinyi amefahamisha kuwa taasisi za Kidini zina wajibu mkubwa wa kushirikiana na Serikali na kuunga Mkono juhudi za kuleta Amani,Umoja na Mshikamano wa Watanzania.

Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba 2024 alipozungumza katika Maombi maalum ya kumpongeza Askofu Agustino Shao kwa utume wake katika Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar na maombi kwa Taifa iliyofanyika Viwanja vya Mao Tse Tung Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk , Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katoliki Jimbo la Zanzibar kwani umekuwa msaada muhimu wa kuimarisha ustawi wa jamii katika nyanja mbalimbali.

Akizungumzia ukarabati wa Kanisa la Minara miwili unaotarajiwa kutekelezwa na Kanisa hilo kuwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali na shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO la kuimarisha Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni Urithi wa Dunia.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amechangia shillingi Millioni Mia moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi Milioni 50 kwa ajili ya Ukarabati wa Kanisa la Mtakatifu Joseph liliopo Shangani Wilaya ya Mjini.

Kwa upande mwingine Rais Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea kuiombea nchi Amani kwani ni nguzo muhimu ya kuleta Umoja ,Amani na Upendo jambo linaloifanya nchi kupiga hatua kubwa za Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages